Mkuu wa Chuo cha Ardhi Morogoro anayo furaha kuwataarifu wahitimu wa mwaka wa masomo 2025/2026, wazazi, walezi, wadau na wananchi wote kuwa Mahafali ya 45 ya Chuo cha Ardhi Morogoro yatafanyika Ijumaa, tarehe 4 Desemba 2026, katika Ukumbi wa Tanzanite Hall, Morogoro, kuanzia saa 3:00 asubuhi. Wote mnakaribishwa kushiriki katika tukio hili muhimu la kitaaluma na maendeleo ya elimu nchini.
Mgeni Rasmi katika sherehe hizi atakuwa Mhe. Dkt. Leonard G. Akwilapo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mahafali haya yanaashiria mafanikio ya wahitimu waliokamilisha masomo yao katika programu mbalimbali zinazotolewa na Chuo cha Ardhi Morogoro, zikiwemo Geomatics, GIS na Urban and Regional Planning (URP). Sherehe hizi pia zinaonesha dhamira ya Chuo ya kuandaa wataalamu wenye uwezo wa kuchangia maendeleo endelevu ya Taifa kupitia elimu na ubunifu.
Taarifa Muhimu kwa Wahitimu
Wahitimu wote wanaotarajia kushiriki mahafali wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya tarehe 2 Desemba 2026 kupitia namba ya simu 0659 408 018.
Mazoezi ya mahafali yatafanyika Alhamisi, tarehe 3 Desemba 2026.
Mawasiliano
Tovuti: www.arimo.ac.tz
Barua pepe: info@arimo.ac.tz
Chuo cha Ardhi Morogoro
Elimu Inaijenga Kesho Yetu