Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa – Mkupuo wa Septemba 2026/2027 (First Round)

Chuo cha Ardhi Morogoro (ARIMO) kinabaki kuwa kinara katika elimu ya upimaji ardhi, uandaaji ramani, upangaji miji, na usimamizi wa ardhi. Kwa furaha kubwa, Chuo kinatangaza rasmi orodha ya wanafunzi wapya waliochaguliwa kujiunga na programu za NTA Level 4 na Level 5 kwa mwaka wa masomo 2026/2027 – First Round.

Jumla ya wanafunzi 266 wamechaguliwa katika programu zifuatazo:

Geographical Information System (GIS)

Geomatics

Land Management, Valuation and Registration (LMVR)

Urban and Regional Planning (URP)

Orodha kamili ya wanafunzi imechapishwa na inapatikana kwenye tovuti ya Chuo kwa ajili ya marejeo.

Chuo kinawapongeza wote waliofanikiwa na kuwahimiza kujiandaa kwa safari ya kujenga ujuzi, ubunifu, na taaluma imara katika sekta ya ardhi.

Karibuni ARIMO – Jenga Baadaye Yako!