MATOKEO YA UHAKIKI WA UDAHILI AWAMU YA KWANZA KWA MWAKA WA MASOMO 2022/2023

Posted On: 26, September 2022

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limetangaza matokeo ya uhakiki wa sifa za waombaji wa programu mbalimbali awamu ya kwanza katika Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa Mwaka wa Masomo 2022/2023 tarehe 24 Septemba, 2022.

Maombi ya nafasi za masomo kwa mwaka 2022/2023 yalianza tarehe 24 Mei, 2022 hadi tarehe 30 Agosti, 2022. Waombaji wa kozi za Astashahada na Stashahada walituma maombi ya kudahiliwa katika Vyuo mbalimbali Tanzania Bara na Visiwani. Vyuo vilipokea maombi na kuchagua waombaji kulingana na sifa za programu zinazotolewa na vyuo hivyo.

Waombaji waliohakikiwa na kuonekana kuwa hawakukidhi vigezo kwenye programu walizoomba wanashauriwa kuomba upya awamu ya pili kati ya tarehe 24 hadi 03 Oktoba, 2022 moja kwa moja Vyuoni kulingana na vigezo katika programu husika. Baraza linawashauri wale ambao hawakuomba katika awamu ya kwanza kufanya hivyo katika awamu ya pili.

Aidha, majina ya waombaji watakaochaguliwa katika awamu ya pili yatawasilishwa NACTVET kuhakikiwa kuanzia tarehe 30 Septemba hadi 08 Oktoba, 2022. Matokeo ya uhakiki huo yatatolewa ifikapo tarehe 17 Oktoba, 2022. Masomo kwa waliochaguliwa yataanza rasmi tarehe18 Oktoba, 2022

Wanafunzi walioomba kusoma kozi za Jiomatikia na Mipango Miji katika Chuo cha Ardhi Morogoro wanaweza kuona matokeo hayo katika tovuti hii kwa link zifuatazo:

1. STUDENTS' VERIFICATION IN BASIC TECHNICIAN CERTIFICATE IN GEOMATICS_2022_2023

2. STUDENTS' VERIFICATION IN BASIC TECHNICIAN CERTIFICATE IN URBAN AND REGIONAL PLANNING_2022_2023

3. STUDENTS' VERIFICATION IN TECHNICIAN CERTIFICATE IN GEOMATICS_20222023

4. STUDENTS' VERIFICATION IN TECHNICIAN CERTIFICATE IN URBAN AND REGIONAL PLANNING_2022_2023