Mkuu wa Chuo cha Ardhi Morogoro anawaalika wahitimu wa mwaka wa masomo 2024/2025 pamoja na wadau wote kushiriki katika sherehe za mahafali ya arobaini na nne (44) zitakazofanyika siku ya Ijumaa, tarehe 12 Desemba 2025, kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Mgeni rasmi wa mahafali haya anatarajiwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Dkt. Leonard G. Akwilapo.
Maelekezo kwa Wahitimu
1) Wahitimu wote wanaotarajia kushiriki sherehe hizi wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya tarehe 10 Desemba 2025 kupitia namba ya simu: 0659 643 333.
2) Wakati wa kuthibitisha, wahitimu wanatakiwa kutaja majina kamili na programu walizohitimu.
3) Aidha, wahitimu wote wanatakiwa kufika chuoni tarehe 11 Desemba 2025 kwa ajili ya mazoezi ya mahafali.
Karibu Wote
Sherehe hizi ni za heshima na furaha kwa chuo, wahitimu, na wadau wote wa sekta ya ardhi. Wote mnakaribishwa.